1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shanghai. Japan yataka kuombwa radhi rasmi na China kutokana na maandamano yaliyosababisha uharibifu kwa biashara za Wajapa nchini China.

17 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFMJ

Japan imetoa malalamiko rasmi na kudai kuombwa radhi baada ya waandamanaji nchini China kufanya ghasia mjini Shanghai. Kiasi cha waandamanaji 10 000 waliandamana wakiipinga Japan dhidi ya vitendo vyake wakati wa vita. Ulinzi katika maeneo ya biashara za Wajapani uliimarishwa wakati waandamanaji wakipita nje ya ubalozi mdogo wa Japan mjini Shanghai, wakitupa mawe na chupa.

Watu wengine 10 000 waliandamana mjini Hangzhou jana wakitoa wito wa kususia bidhaa za Japan. Wachina wengi wamekasirishwa na kuandikwa kitabu ambacho wanasema kinaondoa makosa yote yaliyofanywa na Japan nchini China wakati wa vita vikuu vya pili vya dunia. Pia wanapinga juhudi za Japan za kutaka kupata kiti cha kudumu katika baraza la usalama la umoja wa mataifa.