1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Shambulizi la Ukraine lateketeza kituo cha mafuta cha Urusi

28 Julai 2024

Shambulizi la droni la Ukraine katika eneo la Kursk nchini Urusi limesababisha kuteketea kwa kituo cha kuhifadhi mafuta. Haya yameripotiwa mapema Jumapili na gavana wa eneo hilo.

https://p.dw.com/p/4ipmX
Shambulizi la droni la Ukraine lateketeza kituo cha kuhifadhi mafuta katika eneo la Kursk nchini Urusi mnamo Februari 15, 2024
Moto wateketeza kituo cha kuhifadhi mafuta katika eneo la Kursk nchini UrusiPicha: Handout/TELEGRAM/@gubernator_46/AFP

Kupitia ujumbe alioandika kwenye mtandao wa kijamii wa Telegram, kaimu gavana Alexei Smirnov, amesema matangi matatu ya mafuta yameshika moto na juhudi za kuzima moto huo zinaendelezwa.

Hata hivyo Smirnov ameongeza kuwa hakuna mkazi ama mfanyakazi katika eneo hilo aliyejeruhiwa.

Maeneo mengine ya Urusi pia yashambuliwa

Wizara ya ulinzi mjini Moscow pia imeripoti kuhusu mashambulizi kadhaa ya droni katika maeneo mengine ya Urusi, ikiwa ni pamoja na mkoa wa Kursk, ambao mara kwa mara hulengwa na mashambulizi.

Soma pia;Zelensky asema wanajeshi wake wanakabiliwa na wakati mgumu katika uwanja wa mapambano

Kulingana na Smirnov, taka kutoka kwa droni iliyoanguka ziligonga nyumba moja katika

kijiji kilichoko mkoa wa Kursk, ambacho baadaye kilishika moto. Hakuna mtu

alijeruhiwa. Katika mji mdogo wa Sudzha, droni ya Ukraine iliangusha kifaa cha kulipuka kwenye jengo moja la makazi na kumjeruhi mwanamke mmoja.