1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Shambulizi la Israel lawaua watu 40

10 Septemba 2024

Shambulizi la Israel kwenye kambi ya Wapalestina waliokimbia makazi yao kutokana na vita huko Gaza, limewaua watu 40 na kuwajeruhi wengine 60 mapema siku ya Jumanne.

https://p.dw.com/p/4kS6F
Ukanda wa Gaza | Mpiga picha wa AFP Mahmoud Hams
Mwandishi wa habari akiangalia jengo lililoanguka kufuatia shambulizi la Israel katika Ukanda wa GazaPicha: AFP

Maafisa wa Palestina wamethibitisha idadi ya vifo hivyo.

Israel imedai kuwa inawalenga wanamgambo wakuu wa Hamas, madai ambayo yamekanushwa na kundi hilo. Shambulio hilo ni miongoni mwa mashambulizi mabaya zaidi kuwahi kutokea katika eneo la Muwasi lenye kambi za mahema zenye msongamano wa watu katika mwambao wa Gaza.

Israel ilitenga eneo hilo kuwa eneo la kibinadamu kwa maelfu ya watu wanaotafuta hifadhi kutokana na vita vya Israel na Hamas. Israel inadai kwamba inajizuia kuwadhuru raia wakati wa mashambulizi yake na kuwatuhumu Hamas kwa vifo vya raia kwasababu mara nyingi wanaendesha harakati zao katika maeneo ya makazi.