1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Shambulio la Urusi laua watu 4 karibu na mji wa Donetsk

22 Julai 2023

Takriban watu wanne wameuwawa kwenye kijiji cha Nyu-York mjini Donetsk katika shambulio la hivi karibuni lililofanywa na majeshi ya Urusi mashariki mwa Ukraine.

https://p.dw.com/p/4UG6j
Krim, Kirovske | Brand auf Militärgelände
Picha: Stringer/REUTERS

Taarifa hiyo imetolewa Jumamosi na ofisi ya mwendesha mashtaka ya mji huo ambapo taarifa zaidi zinasema kuwa vikosi vya Urusi vilidondosha mabomu chapa Fab 250 Ijumaa jioni. Raia watatu waliojeruhiwa katika tukio hilo wamepelekwa hospitali kwa matibabu.

Katika hatua nyingine, Gavana wa rasi ya Crimea Sergei Aksyonov amesema Ukraine ilijaribu kufanya shambulizi kwa kutumia ndege isiyo na rubani katika eneo hilo mapema leo. 

Soma pia: Idadi ya waliuwawa kwenye mashambulizi ya Urusi yaongezeka

Gavana huyo amesema shambulio hilo lililenga miundombinu ya wilaya ya Krasnohvardiiske karibu na eneo la katikati mwa rasi ya Crimea.

Awali shirika la habari la Urusi kupitia ukurasa wake wa Telegram liliripoti kusimama kwa usafiri wa barabara katika daraja linayoiunganisha Urusi na rasi hiyo bila kuainisha sababu za hatua hiyo. Lakini baadaye iliripotiwa kwamba shughuli za usafiri kwenye daraja hilo sasa zinaendelea kama kawaida.