1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shambulio la Israel lawaua wapiganaji wa Hezbollah

9 Agosti 2024

Jeshi la Israel limesema leo kuwa limewaua wapiganaji wawili wa kundi la wanamgambo la Hezbollah kusini mwa Lebanon, huku kundi hilo lenye kuungwa mkono na Iran likithibitisha vifo vya wanachama wake watatu.

https://p.dw.com/p/4jIe4
Libanon I Israelischer Luftangriff
Picha: Stringer/REUTERS

Taarifa za mauaji hayo hata hivyo hazijathibishwa na vyanzo huru.

Jeshi la Israel limeeleza kuwa limefanya shambulio katika kambi ya Hezbollah eneo la Naquora, umbali mdogo na mpaka wa Israel.

Kundi la Hezbollah wakati linathibitisha vifo vya wanachama wake watatu, halikusema sehemu au wakati vifo hivyo vilivyotokea badala yake limedai kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi kaskazini mwa Israel.

Hezbollah na wanajeshi wa Israel wamekuwa wakipigana karibu kila siku tangu mzozo kati ya Hamas na Israel ulipoanza mnamo mwezi Oktoba.