1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Shambulio la anga la Israel laua wapiganaji wawili wa Iran

12 Machi 2023

Shirika la haki za binadamu la Syria lenye makao makuu yake nchini Uingereza limesema mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Israel na ambayo yalilenga ghala la silaha yamewaua wapiganaji wawili wanaoiunga mkono Iran.

https://p.dw.com/p/4OZ1n
Israel | Palästinenser | Raketenangriffe aus dem Gzsastreifen
Picha: Ariel Schalit/AP Photo/picture alliance

Shirika la haki za binadamu la Syria lenye makao makuu yake nchini Uingereza limesema mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Israel na ambayo yalilenga ghala la silaha nchini Syria yamewaua wapiganaji wawili wanaoiunga mkono Iran na kuwajeruhi wanajeshi watatu wa Syria.

Shirika la habari la serikali ya Syria, SANA, lililokinukuu chanzo cha jeshi, limeripoti kuwa Israel imefanya shambulio la anga kutokea upande wa kaskazini mwa Lebanon na kulenga wilaya za Tartus na Hama.

Jeshi la Israel, hata hivyo, halikuzungumzia juu ya shambulio hilo lililoripotiwa kwenye "vyombo vya habari vya kigeni."

Ni nadra sana kwa jeshi la Israel kuzungumzia juu ya mashambulizi wanayoyafanya dhidi ya Syria, japo limeapa kuendelea na mashambulizi ya anga ili kuzuia adui yake Iran kuimarisha uwepo wake nchini humo.