1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali ya Ujerumani yapata mwafaka kuhusu bajeti ya 2024

13 Desemba 2023

Serikali ya Muungano ya Ujerumani inayoongozwa na Kansela Olaf Scholz, imekubaliana kuhusu bajeti ya mwaka 2024.

https://p.dw.com/p/4a6Jx
Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani.
Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani.Picha: Bernd von Jutrczenka/dpa/picture alliance

Hii ni kufuatia mazungumzo ya wiki kadhaa, baada ya uamuzi wa mahakama mwezi uliopita uliotupilia mbali makadirio hayo na kuzusha mtafaruku.

Kulingana na vyanzo vitatu vya serikali ambavyo vimezungumza na shirika la habari la Reuters mapema leo, serikali itawasilisha makadirio hayo ya bajeti baadaye leo bungeni.

Mnamo Novemba 15, mahakama ya kikatiba ya Ujerumani iliamua kwamba uamuzi wa serikali kutenga euro bilioni 60 ya deni ambalo halikutumika katika janga la COVID-19, kuelekeza kwenye Mfuko wake wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa ulikuwa kinyume na katiba.