1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali ya Ruto kurejesha vipengee vya mswada wa fedha

19 Agosti 2024

Serikali ya Kenya imesema italazimika kurejesha baadhi ya hatua za ulipaji kodi ambazo zilifutwa baada ya kuibuka maandamano makubwa mwezi Juni.

https://p.dw.com/p/4jeB8
William Ruto, rais wa Kenya
William Ruto, rais wa KenyaPicha: Thomas Mukoya/REUTERS

Hatua ya serikali ya Kenya ni jambo linalozidisha hatari ya kutokea machafuko zaidi katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Fedha wa nchi hiyo John Mbadi aliyesisitiza kwamba baadhi ya hatua zitarekebishwa, lakini akasema zinahitajika ili kumudu matumizi ya serikali ikiwa ni pamoja na kulipa mishahara ya walimu.

Baada ya kauli hiyo ya Waziri Mbadi aliyoitoa jana usiku wakati wa mahojiano na kituo cha televisheni cha CItizen, baadhi ya watu walioshiriki maandamano yaliyoongozwa na vuguvugu la vijana maarufu kama Gen-Z wamesema wako tayari kuingia tena mitaani na kuandamana.