Serikali ya mseto yatangazwa Kenya.
14 Aprili 2008Matangazo
NAIROBI:
Rais Mwai Kibaki wa Kenya ametangaza baraza jipya la mawaziri 42 ikiwa ni hatua ya kumaliza mgogoro wa kisiasa uliokuwa unaikabili Kenya kufuatia kutangazwa matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika mwezi desemba mwaka jana.
Rais Kibaki pia amemtangaza rasmi kiongozi wa upinzani wa chama cha ODM Raila Odinga kuwa waziri mkuu.
Akitangaza baraza hilo ikiwa ni hatua iliyofikiwa chini ya makubaliano ya kugawana madaraka na upande wa upinzani, bwana Kibaki amewataka wakenya waweke kando siasa ili waanze kufanya kazi ya kuijenga nchi yao.
Katika baraza hilo,bwana uhuru Kenyatta wa chama kinachotawala PNU na bwana Musalia Mudavadi wa chama cha upinzani, ODM watakuwa makamu wa waziri mkuu.