1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaJamhuri ya Moldova

Serikali ya Moldova yavunjika

10 Februari 2023

Serikali ya Moldova imevunjika baada ya Waziri Mkuu mwenye kuegemea upande wa Magharibi, Natalia Gavrilita kujiuzulu.

https://p.dw.com/p/4NKrD
Ex-Premierministerin der Republik Moldau Natalia Gavrilita
Picha: Elena Covalenco /DW

Hatua hiyo inaongeza mfululizo wa migogoro unayoligubika taifa hilo dogo, tangu Urusi ilivamie taifa jirani yake, Ukraine.

Akitangaza hatua hiyo mbele ya waandishi wa habari,Gavrilita amesema hakuna aliyetarajia kwa serikali yake iliyochaguliwa kipindi cha kiangazi cha mwaka 2021, ingemudu kutatua migogoro mingi iliyosababisha na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Uongozi wake uligubikwa na mkururo wa matatizo, ikiwemo shida ya nishati, mfumuko wa bei unaoongezeka na kadhia nyingine kama kuvuka kwa makombora katika anga yake kutoka uwanja wa vita huko Ukriane.

Serikali mpya itateuliwa na Rais Maia Sandu na baadae itahitaji kuidhinishwa na bunge la Moldova lenye wajumbe 101.