1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali ya mashariki Libya yaitaka Misri kuingilia vita

14 Julai 2020

Serikali ya mashariki mwa Libya imeiomba Misri kuingilia kati kijeshi katika vita vya wenyewe kwa wenyewe, ili kukabiliana na vikosi vya Uturuki vinvaoiunga mkono serikali ya GNA.

https://p.dw.com/p/3fI3A
Libyen Tripoli | Portrait | GNA Kämpfer
Picha: picture-alliance/dpa/A. Salahuddien

Katika taarifa iliyotolewa Jumatatu, bunge hilo linalojulikana kama Baraza la wawakilishi lenye makao yake katika mji wa bandari wa Mashariki wa Tobruk, ilisema msaada wa Misri unahitajika ili kukabiliana na kile lilichokitaja kuwa uvamizi na ukaliaji wa Uturuki.

Soma zaidi: Guterres alaani uingiliaji wa kigeni Libya

Taarifa hiyo inatilia mkazo hatari inayozidi nchini Libya, ambako pande mbili zimejiimarisha kimapambano mapema mwezi huu karibu na mji wa Sirte, baada ya serikali ya Tripoli GNA inayotambuliwa kimataifa, pamoja na Uturuki kuwafurusha wapiganaji wa mashariki wa kundi linalojiita Jeshi la Taifa la Libya LNA, baada ya mwaka mzima wa mashambulizi dhidi ya Tripoli.

Libya imegawika tangu mwaka 2014 kati ya serikali ya Maridhiano ya kitaifa GNA mjini Tripoli na utawala hasimu mjini Benghazi, ambako kamanda wa LNA Khalifa Haftar anahodhi mamlaka. Pia kuna baraza tofauti la wawakilishi lenye makao yake mjini Tripoli. Mzozo mkubwa mwingine unahatarisha kuzusha mgogoro wa moja kwa moja nchini Libya miongoni mwa mataifa ya kigeni ambayo tayari yamemuaga silaha na wapiganaji katika ukiukaji wa marufuku ya silaha. Kikosi cha LNA kinaungwa mkono na Misri, Umoja wa Falme za Kiarabu na Urusi.

Karte Libyen UAE Türkei EN
Ramani inayoonesha Libya na Uturuki

Soma zaidi:Misri iko tayari kuingilia kati vita vya Libya

Rais wa Misri, Abdel Fttah el-Sisi ameonya tayari kwamba jeshi lake linaweza kuingia Libya ikiwa GNA na washirika wake wa Uturuki wataendeleza mashambulizi dhidi ya Sirte, ambao ni mji wa pwani unaotazamwa kama njia kuu ya usafirishaji wa mafuta ya Libya. Udhibiti wa mafuta, ambayo ndiyo chanzo kikuu cha mapato ya serikali, umeibuka kuwa zawadi kuu katika mgogoro huo, ambapo vikosi vya mashariki vimeweka mzingiro kwenye uchimbaji na usafirishaji nje wa nishati hiyo tangu mwezi Januari.

Chini ya makubaliano ya kimataifa, ni shirika la taifa la mafuta NOC pakee, lenye makao yake mjini Tripoli, lina haki ya kuzalisha na kusafirisha mfuta, huku mapato yakitakiwa kupitia benki kuu ya Libya, ambayo pia iko mjini Tripoli. Siku ya Ijumaa, juhudi za kidiplomasia zinazoongozwa na Umoja wa Mataifa na Marekani, zilionekana kukomesha mzingiro wa mafuta baada ya meli ya kwanza kuruhusiwa kutia nanga katika bandari ya Es Sider na kupakia mafuta.

Hata hivyo, LNA ilisema siku ya Jumamosi kwamba ilikuwa inarejesha mzingiro, katika umuazi ambao shirika la mafuta la NOC, liliulamu kwa Umoja wa Falme za Kiarabu, UAE. UAE ilisema inataka kurejea haraka kwa mauzo ya nje ya mafuta, lakini iwapo tu masharti yatatimizwa.

Chanzo: rtrte