1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali ya Hungary yakabiliwa na maandamano ya kuipindua

19 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDAu

Maelfu kadhaa ya watu wameandamana mbele ya bunge la Hungary katika mji mkuu Budapest wakimtaka waziri mkuu Ferenc Gyurcsany kutoka chama cha kisosialist ajiuzulu. Kuna wengine ambao wamevamia televisheni ya taifa na kuyachoma moto magari. Taarifa zinasema kuwa watu 150 wakiwemo polisi 100, wamejeruhiwa katika ghasia ambazo zimezuka kati ya waandamanaji na polisi.