1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SERIKALI MPYA NCHINI BURUNDI:

24 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CFyd

BUJUMBURA: Rais Domitien Ndayizeye wa Burundi ameunda serikali mpya iliyomuingiza Pierre Nkurunziza-kiongozi wa zamani wa kikundi kikubwa kabisa cha waasi wa Kihutu FDD.Wanachama wengine 3 wa FDD pia wameteuliwa kama mawaziri.Tangazo hilo limetolewa wiki moja baada ya kutiwa saini makubaliano ya amani,kati ya rais Ndayizeye na bwana Nkurunziza.Mkataba huo wa amani ulitiwa saini nchini Tanzania kwenye mkutano wa kilele wa kanda hiyo kwa lengo la kukomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu miaka 10.Chama kingine cha waasi FNL kilichopewa muda wa miezi mitatu kuweka chini silaha zake na hivyo kumaliza vita,kimekataa kutekeleza muito huo.Kiasi ya watu 300,000,wengi wao ikiwa ni raia,wamepoteza maisha yao katika vita vilivyozuka tangu kuuawa kwa rais Melchior Ndadaye,na jeshi lililotawaliwa na Watutsi walio wachache.Ndadaye alikuwa rais wa kwanza wa Burundi aliekuwa Mhutu.