1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali mpya imeapishwa Ugiriki

12 Novemba 2011

Baraza jipya la mawaziri katika serikali ya mpito limeapishwa likiongozwa na waziri mkuu mpya Lucas Papademos

https://p.dw.com/p/139UP
Kiongozi mpya wa serikali Ugiriki, Lucas PapapdemosPicha: picture alliance/dpa

Waziri mkuu huyo mpya aliyechaguliwa, alitangaza kuwa serikali mpya itajitahidi kukabiliana na matataizo ya nchi hiyo.

Griechenland Neues Kabinett November 2011
Lucas Papademos, akiapishwa rasmi nchini UgirikiPicha: dapd

Mwanasiasa Evangelos venizelos anasalia kuwa waziri wa fedha pamoja na kuwa naibu waziri mkuu. serikali hiyo mpya ya mseto inajumuisha mawaziri kutoka vyama viwili vikuu nchini humo ambayvo ni chama cha kisoshalisti na cha kihafidhina, na pia kutoka chama kidogo cha mrengo wa kulia.

katika sherehe zilizofana zilizoongozwa na kasisi mkuu wa nchi hiyo, Papademos na baraza hilo jipya la mawaziri walibarikiwa wakati wanapoanza majukumu mapya ya kuutatua mzozo wa nchi hiyo.

Baada ya majadiliano ya siku nne vyama viwili vikuu nchini humo vilikubaliana siku ya Alhamisi kumchagua Papademos ambaye ni kiongozi wa kujitegemea kuwa mkuu wa serikali hiyo mpya ya muungano.

Na wakati wanasiasa nchini humo walikuwa katika harakati za kushinikiza hatu hizo za kubana matumizi na kuinda serikali hiyo mpya, Papademos alisema kuwa lengo lake litakuwa ni kufikia masharti yaliotolewa na Umoja wa Ulaya na shirika la fedha la kimataifa IMF, ili kupokea mkopo mwingine kwa nchi hiyo na kuiokoa dhidi ya kufilisika.

Griechenland Finanzkrise George Papandreou zurückgetreten
Waziri mkuu aliyejiuzulu George PapandreouPicha: dapd

Katika mkutano wake wa kwanza na serikali hiyo mpya, waziri mkuu huyo alieleza kuwa matokeo ya mwisho yatategemea iwapo nchi hiyo itafanikiwa kuiarisha uchumi wake, kukabiliana na ukosefu wa ajira na kudhinisha njia za kuufufua uchumi katika muda mfupi.

Wachambuzi wanasema kiongozi huyo mpya ambaye ni mwanauchumi, ni lazima ashinize uongozi wake dhidi ya baraza hilo jipya linalojumuisha wanachama wa chama hicho cha kihafidhina na cha kisoshalisti ambavyo vilibadilishana zamu katika uongozi kwa miongo kadhaa, wakati nchi hiyo ilipojilimbikizia deni hilo kubwa ambalo ilishindwa kulidhibiti na kulazimisha kutafuta mkopo wa kimataifa.

Athens inahitaji fedha kwa haraka kutoka kwa shirika la fedha la kimataifa IMF na Umoja wa Ulaya ili iweze kulipa madeni yake kufikia mwezi ujao Disemba la sivyo ishindwe kulilipa deni hilo, na iishie kufilisika na kukabiliwa pia na hatari ya kujitoa katika nchi zinazoitumia sarafu ya euro.

Europa Griechenland Krise
Bunge la UgirikiPicha: dapd

Waziri wa fedha Evangelos Venizelos amesema jitihada za kupata mkopo huo wa dharura ndiyo lengo kuu la kwanza la serikali hiyo mpya.

Duru zimeeleza kuwa wakaguzi wa Umoja wa Ulaya, IMF na Benki kuu ya Ulaya wataizuru Athens mapema wikiijayo kuzungumza na serikali hiyo mpya na kutoa fungu hilo la fedha iwapo serikali itaahidi kufikia masharti yao.

Lucas Papademos ataiongoza serikali hiyo mpya ya mpito hadi uchaguzi utakapoitishwa baadaye mwaka ujao.

Mwandishi: Maryam Abdalla/ Rtre/DPAE
Mhariri: Kitojo Sekione