1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSerbia

Serbia, Kosovo washindwa kurejesha uhusiano wa kidiplomasia

19 Machi 2023

Viongozi wa Kosovo na Serbia wameshindwa jana kutia saini makubaliano ya kurejesha uhusiano wao wenye utata wakati wa mazungumzo yaliyofanywa chini ya usaidizi wa Umoja wa Ulaya.

https://p.dw.com/p/4Oto0
Kombobild I Aleksandar Vucic und Albin Kurti,
Picha: Darko Vojinovic/AP/picture alliance / Boris Grdanoski/AP/picture alliance

Waziri Mkuu wa Kosovo Albin Kurti na Rais wa Serbia Aleksandar Vucic walikutana kwa mazungumzo ya saa 12 kwenye mwambao wa Ziwa Ohrid, huko Macedonia Kaskazini, chini ya usaidizi wa mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell. Umoja wa Ulaya hata hivyo umepongeza maendeleo yaliyofikiwa.

Soma pia: Mkutano wa Serbia na Kosovo umemalizika bila maafikiano

Katika miezi ya hivi karibuni, mataifa ya Magharibi yamekuwa yakiongeza shinikizo kwa Belgrade na Pristina ili kutatua mzozo wao na kuzuia uwezekano wa kuzuka kwa mvutano katika eneo tete la Balkan wakati uvamizi wa Urusi ukiendelea huko Ukraine.

Serbia inakataa kuutambua uhuru wa jimbo lake la zamani la Kovoso uliotangazwa mwaka 2008.