1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSerbia

Serbia, Kosovo wakutana kwenye mazungumzo ya kusakaa suluhu

14 Septemba 2023

Viongozi wa Serbia na Kosovo wanakutana katika awamu mpya ya mikutano hii leo inayolenga kuimarisha mahusiano yaliyoharibika.

https://p.dw.com/p/4WKPU
Rais wa serbia Aleksandar Vucic
Rais wa serbia Aleksandar VucicPicha: OLIVER BUNIC/AFP/Getty Images

Rais wa Serbia Aleksandar Vucic na waziri mkuu wa Kosovo Albin Kurti wako Brussels kwa mazungumzo chini ya kile kinachoitwa mchakato wa mazungumzo wa Belgrade-Pristina, unaosimamiwa na mkuu wa sera za kigeni wa Ulaya, Josep Borrell.

Mikutano hii inafanyika hukumiito ikiongezeka ya mabadiliko katika mchakato wa kidiplomasia wa magharibi katika kuushughulikia mvutanouliopo, huku kukiwa na mashaka huenda ukasambaa na kushindwa kudhibitiwa.

Soma pia:Serbia yawaachia maafisa wa polisi wa Kosovo

Awamu ya mwisho ya mazungumzo mwezi Juni ilimalizika bila ya makubaliano yoyote.

Vucic na Kurti walikataa kukutana ana kwa ana na Borrell aliyekutana nao kwa nyakati tofauti alikiri kwamba wakuu hao walikuwa na "tafsiri tofauti za sababu, ukweli, matokeo na suluhisho la mvutano huo uliodumu kwa miongo kadhaa.