1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUholanzi

Sera ya Uhamiaji yaiangusha serikali ya Uholanzi

8 Julai 2023

Waziri Mkuu wa Uholanzi Mark Rutte ametangaza kujiuzulu usiku wa kuamkia leo baada ya kuanguka kwa serikali yake ya mseto ya vyama vinne kutokana na tofauti kubwa juu ya sera ya uhamiaji.

https://p.dw.com/p/4TcOf
Waziri Mkuu wa Uholanzi Mark Rutte
Waziri Mkuu wa Uholanzi Mark RuttePicha: Robin Utrecht/dpa/ANP/picture alliance

Rutte amesema tofauti zilizojitokeza kuhusu sera hiyo baina ya vyama washirika haziwezi kurekebishwa na kwamba uamuzi wa kuivunja serikali ulikuwa wa lazima. Hii leo Rutte amepangiwa kuwa na mkutano na Mfalme Willem-Alexander kumwarifu rasmi uamuzi wake wa kujiuzulu na inatarajiwa uchaguzi mpya utaandaliwa mwezi Novemba.

Chanzo cha mvutano ni pendekezo la chama cha Rutte cha VVD kinachoegemea siasa za mrengo wa kulia la kutaka kuzuia wahamiaji walio nchini Uholanzi kujiunga na familia zao.

Pendekezo hilo linapingwa vikali na chama cha kihafidhina cha Christian Unioni kinachotaka uwepo uwezekano wa kuwaruhusu watoto wa wakimbizi wa vita kujiunga na wazazi wao nchini Uholanzi.