1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Seoul. Wanasayansi wapata mafanikio katika utafiti wa chembe za uhai kwa ajili ya matibabu ya ugonjwa kama wa kisukari na kutetemeka.

21 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFBt

Wanasayansi wa Korea ya kusini wamesema kuwa wamepata mafanikio katika utafiti wao wa chembe ya uhai ambayo inaweza kupelekea kupatikana matibabu ya magonjwa yanayoathiri maisha.

Watafiti hao wanasema kuwa wamefanikiwa kutoa kiumbe ambacho kimetokana na kiumbe kimoja bila ya kujamiiana na kingine, kwa mara ya kwanza, na kupata chembe za uhai ambazo zitafanana na kiumbe kinachokusudiwa.

Mafanikio hayo ya utafiti kuhusu chembe za uhai zinaweza kuwa na maana kuwa kutakuwa na matibabu kwa magonjwa kama kisukari na ugonjwa wa kutetemeka bila matatizo ya mwili kukataa chembe hizo.

Lakini mjini Washington, rais George W. Bush ameeleza wasi wasi wake juu ya utafiti huo wa wanasayansi wa Korea. Pia amerejea maoni yake kuwa anapinga kutolewa fedha za utafiti na serikali kuu kwa masuala ya sayansi kama anavyosema kuwa yanaharibu uhai ili kuokoa uhai.

Bwana Bush amesema kuwa atapinga kwa uwezo wa madaraka yake kupitishwa sheria yoyote ambayo inataka kufanyika utafiti wa aina hiyo.