1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Seoul: Mazungumzo juu ya mpango wa kinyukliya wa Korea kaskazini yataanza karibuni

12 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEvD

Korea Kusini imependekeza kuipatia Korea kaskazini umeme wa moja kwa moja ikiwa nchi hiyo ya kikoministi itaachana na tama yake ya kuwa dola ya kinyukliya. Hapo kabla, serekali ya Korea Kusini ilisema itaipatia Korea Kaskazini tani laki tano za mchele kama msaada baada ya Korea Kaskazini kuamuwa kurejea katika mazungumzo ya nchi sita kuhusu mpango wake wa kuwa na programu ya kinyukliya. Nchi mbili za Korea pia zimekubaliana kuziunganisha tena njia zao za reli kupitia mpaka wao wa pamoja.

Akitembelea Japan, waziri wa mambo ya kigeni wa Japan, Bibi Condeleezza Rice, ameitaka Korea Kaskazini ichukuwe uamuzi muhimu wa kuachana na silaha za kinyukliya. Kwa upande mwengine, Uchina imemtuma mwakiliashi wake maalum, Tang Jiaxuan, hadi Korea Kaskazini kuyatarisha mazungumzo hayo ya nchi sita ambayo yanatazamiwa kuanza tena hapo July 25 baada ya kusita kwa miezi 13.