1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Seoul: Korea Kaskazini yarusha kombora kuelekea Kusini

9 Machi 2023

Korea kaskazini imerusha kombora moja la masafa mafupi kuelekea bahari ya njano kati ya China na rasi ya Korea. Haya ni kwa mujibu wa jeshi la Korea Kusini.

https://p.dw.com/p/4OSyb
Erneuter Raketentest in Nordkorea im November 2022
Picha: KCNA/KNS/STR/AFP

Jeshi hilo limesema kombora hilo limerushwa leo jioni kwa majira ya eneo hilo, katika eneo karibu na mji wa bandari wa Nampo katika Pwani ya Magharibi. Hapo awali, haikujulikana umbali liliporuka kombora hilo.

Korea Kaskazini imepigwa marufuku kufanya majaribio ya makombora ya masafa marefu kutokana na maazimio ya Umoja wa Mataifa.

Tutaijibu Marekani kwa nyuklia - Pyongyang

Kulingana na muundo wake, makombora kama hayo yanawezwa kuwekewa kichwa cha nyuklia . Korea Kaskazini imeongeza wigo na kasi ya majaribio yake ya makombora tangu mwaka jana.