SiasaSenegal
Senegal: Upinzani washtumu mamlaka juu ya tarehe ya uchaguzi
21 Februari 2024Matangazo
Hii ni baada ya mahakama kupitisha uamuzi uliobatilisha hatua ya kuuchelewesha kwa miezi 10 uchaguzi huo.
Rais wa nchi hiyo Macky Sall wiki iliyopita aliahidi kwamba atazingatia ombi lililotolewa na baraza la katiba la kutaka uchaguzi huo upangwe haraka iwezekanavyo.
Mahakama iliitupilia mbali amri ya Rais Macky Sall iliyoungwa mkono na bunge iliyouakhirisha uchaguzi huo uliopangwa awali kufanyika tarehe 25 mwezi huu wa Februari.
Hata hivyo bado tarehe mpya mpaka sasa haijatangazwa hali ambayo imeibuwa wasiwasi miongoni mwa wagombea wa upinzani ambao baadhi wanashinikiza uchaguzi ufanyike kabla ya muhula wa pili wa Rais Macky Sall haujamalizika tarehe 2 mwezi Aprili.