1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Senegal kununuwa mali za Senghor

20 Oktoba 2023

Senegal imetangaza leo Ijumaa kuwa imepanga kuzinunuwa mali za rais wake wa kwanza katika mnada utakaofanyika hapo kesho nchini Ufaransa, ili kuhifadhi kumbukumbu na urithi wa Leopold Sedar Senghor.

https://p.dw.com/p/4Xoy3
DW Thumbnail African Roots Podcast l Composite Bild Oba Ewuare, Sedar Senghor
Picha ya kuchora ikiwaonesha Sedar Senghor (kulia) na Oba Ewuare.

Rais wa sasa wa Senegal, Macky Sall, amemtaka waziri wa utamaduni pamoja na ubalozi wa Senegal mjini Paris, kuanzisha majadiliano muhimu ili kufanikisha zoezi la manunuzi ya vitu hivyo ambavyo ni pamoja na vito na mapambo ya kijeshi vitakavyopigwa mnada mjini Caen.

Soma zaidi: Léopold Sédar Senghor: Mfungwa aliyekuja kuwa rais

Leopold Sedar Senghor aliyekuwa pia mshairi na mwandishi wa vitabu, aliiongoza Senegal kuanzia mwaka 1960 hadi 1980, na alifariki huko Ufaransa akiwa na umri wa miaka 95.

Senghor alikuwa pia Mwafrika wa kwanza kuwa mwanachama wa Baraza la lugha ya Kifaransa, maarufu kama "Academie Francaise".