1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Semenya ashinda rufaa kushiriki michezo ya dunia

11 Julai 2023

Mwanariadha bingwa mara mbili wa Olimpiki, Caster Semenya, ameshinda rufaa dhidi ya sheria za kuwapiga marufuku wanariadha wa kike walio na homoni nyingi za Testerone kushiriki katika mashindano ya dunia.

https://p.dw.com/p/4Tir9
Symbolbild | 800-m-Doppel-Olympiasiegerin Caster Semenya in Südafrika gescheitert
Picha: Karim Jaafar/AFP/Getty Images

Mahakama ya Haki za Binaadamu ya Ulaya imeamua kwamba mwanariadha huyo alibaguliwa.

Uamuzi huo huenda ukailazimisha Mahakama ya Juu zaidi ya michezo kutathmini upya sheria zake zilizomlazimisha Semenya na wanariadha wengine wa kike kupunguza viwango vya homoni za Testerone ili kuruhusiwa kushiriki katika Mashindano ya Olimpiki.

Soma zaidi: Mahakama ya CAS yaanza kusikiliza kesi ya Semenya
Semenya apeperusha Bendera ya Afrika Kusini Olimpik

Mahakama hiyo yenye makao makuu yake mjini Strasbourg, Ufaransa, imeeleza kuwa mwanariadha huyo wa Afrika Kusini alinyimwa haki baada ya Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo kupinga rufaa dhidi ya sheria za kumzuia kushiriki katika mashindano ya dunia.

Hata hivyo, haikubainika mara moja iwapo uamuzi huo utalazimisha kuondololewa kwa sheria hizo na kumruhusu Semenya mwenye umri wa miaka 32 kushiriki katika mashindano ya Olimpiki mwaka ujao mjini Paris.