Scholz na Merz wapambana kwa maneno bungeni
11 Februari 2025Matangazo
Kwenye kikao hicho, Kansela anayewania kuchaguliwa Olaf Scholz wa chama cha SPD amemshambulia kwa maneno mgombea mwenzake wa chama cha kihafidhina cha CDU, Friedrich Merz, akisema mapendekezo yake ya kisera ni "hatari kwa ushirikiano wa kanda ya Ulaya." Amesema sera za CDUzinazoshinikiza Ujerumani ichukue msimamo binafsi kuhusu suala la uhamiaji zinakwenda kinyume na sheria za Ulaya na zitavuruga mshikamano wa kanda hiyo. Kwa upande wake Merz, amekosoa mapendekezo ya Scholz ya kutaka kuongeza kodi kwa matajiri akimtuhumu "kupalalilia wivu na chuki" dhidi ya watu walio na kipato kikubwa. Amezilaumu pia sera za kiuchumi za kiongozi huyo anazosema ndiyo sababu ya kuongezeka idadi ya watu wasio na ajira nchini Ujerumani.