1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bunge la Marekani laombwa kuidhinisha msaada kwa Ukraine

10 Februari 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz na Rais wa Marekani Joe Biden wamewaomba wabunge wa Marekani, kuidhinisha msaada wa kijeshi uliocheleweshwa kwa Ukraine.

https://p.dw.com/p/4cFe1
Kansela Scholz akiwa ziarani, Marekani
Kansela wa Ujerumai Olaf Scholz akiwa na rais wa Marekani Joe Biden.Picha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Viongozi hao wawili, wameonya kuwa taifa hilo haliwezi kuendelea kukabiliana na uvamizi wa Urusi bila msaada huo.

Kansela Scholz ambaye nchi yake ni muungaji mkono mkubwa wa kijeshi wa Ukraine, ikifuatiwa na Marekani amesema anatumai kutafikiwa makubaliano ya kuidhinisha msaada huo wa mabilioni ya dola.

Awali, Scholz aliwaambia waandishi habari kwamba ametiwa moyo na hatua ya Baraza la Seneti la Marekani kuanza kuuangazia mpango utakaoidhinisha msaada wa dola bilioni 60 kwa Kiev.

Biden, Scholz kujadiliana msaada kwa Ukraine

Hata hivyo, bado kuna mashaka ikiwa wabunge wa Republican wanaodhibiti Baraza la Wawakilishi wataupitisha muswada huo.