1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz kwenda Israel kuonesha mshikamano

17 Oktoba 2023

Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani anakwenda Israel kuonyesha mshikamano na nchi hiyo kufuatia shambulzi baya kabisa la kigaidi la Hamas lililofanywa kutokea Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4XcVh
Scholz Bundestag Israel
Picha: Liesa Johannssen/REUTERS

Scholz ni kiongozi wa kwanza wa serikali kwenda Israel tangu shambulizi hilo siku 10 zilizopita.

Alitarajiwa kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu wa Israel kabla kwenda Misri ambako atakutana na Rais Abdel Fattah al-Sissi wa nchi hiyo.

Kansela Sholz alisema anataka kujadili hali katika uwanja wa vita na jinsi ya kuepusha machafuko zaidi.

Soma zaidi: Scholz: Ujerumani kupiga marufuku shughuli za Hamas

Mazungumzo yake pia yalitarajiwa kuhusu njia za kuwakomboa mateka kiasi 200 wanaoshikiliwa na Hamas, wakiwemo Wajerumani na juhudi za kuepusha vita kamili Mashariki ya Kati.

Scholz alitarajiwa kutangaza msaada wa kijeshi kwa Israel na msaada wa kibinaadamu kwa watu wa Gaza.

Ziara ya Scholz nchini Israel ilitanguliwa na mkutano wake Mfalme Abdullah wa Pili wa Jordan mjini Berlin.