1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz kukutana na wawakilishi wa wakulima Alhamisi

Josephat Charo
10 Januari 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz anatarajiwa kufanya mazungumzo na wawakilishi wa jumuiya ya wakulima kuhusu maandamano yao ya kupinga kupunguzwa kwa ruzuku ya kodi ya mafuta ya dizeli kwa ajili ya kilimo.

https://p.dw.com/p/4b5jv
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz
Kansela Olaf Scholz anakabiliwa na shinikizo kubwa kutatua matatizo chungumzima.Picha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz anatarajiwa kufanya mazungumzo na wawakilishi wa jumuiya ya wakulima kuhusu maandamano yao ya kupinga kupunguzwa kwa ruzuku ya kodi ya mafuta ya dizeli kwa ajili ya kilimo.

Msemaji wa serikali Steffen Hebestreit amesema hivi leo mjini Berlin kwamba kansela Scholz anapanga kukutana na kiongozi wa wakulima wa jimbo la Brandenburg kesho Alhamisi kandoni mwa hafla ya ufunguzi wa kituo kipya cha treni itakayofanyika mjini Cottbus.

Soma pia: Je, mgomo wa madereva wa treni unaathiri vipi usafiri wa mizigo?

Hebestreit amesema Scholz anataka kwa mara nyingine tena kufafanua msimamo wa serikali. Chama cha wakulima katika jimbo la Brandenburg kimesema wakulima wanataka kufanya maandamano mjini Cottbus.