1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz awasili Israel

17 Oktoba 2023

Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani amewasili nchini Israel katika ziara inayolenga kuonyesha mshikamano kufuatia shambulizi baya la kigaidi la Hamas.

https://p.dw.com/p/4XeRz
Israel Tel Aviv | Ankunft Bundeskanzler Scholz zu Solidaritätsbesuch
Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani akiwasili nchini Israel kuonesha mshikamano.Picha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Scholz anatarajiwa kufanya mazungumzo na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu mjini Tel Aviv.

Anatarajiwa pia kukutana na Rais wa Israel Isaac Herzog na jamaa wa mateka wanaoshikiliwa na Hamas, wakiwemo raia kadhaa wa Ujerumani, kabla kusafiri kwenda Misri ambako atakutana na Rais Abdel Fattah al-Sissi.

Soma zaidi: Scholz: Ujerumani kupiga marufuku shughuli za Hamas

Biden kuizuru Israel wakati ikijiandaa kuivamia Gaza

Kansela Scholz anapanga kujadili hali katika uwanja wa vita na jinsi ya kuepusha mzozo kuongezeka.

Wakati haya yakiarifiwa Rais wa Marekani Joe Biden naye anatarajiwa kuwasili Israel kesho Jumatano kujaribu kuepusha vita dhidi ya Hamas kuwa vikali huko Gaza na kutanuka kuwa mzozo mpana wa Mashariki ya Kati.