1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani na juhudi za kuwa mwenyeji wa soka la wanawake

22 Februari 2023

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, ameonesha nia madhubuti ya kuunga mkono juhudi za kusaidia Ujerumani kuwa mwenyeji wa maandalizi ya Kombe la Dunia la Wanawake kwa 2027, sambamba na Uholanzi na Ubelgiji.

https://p.dw.com/p/4NooB
Empfang der deutschen Nationalmannschaft der Frauen auf dem Frankfurter Römer WM 2007
Picha: AP

Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa Rais wa Shirikisho la Soka la Ujerumani, DFB, Bernd Neuendorf.

Uteuzi wa taifa mwenyeji wa michuano hiyo ya Kombe la Kandanda la Dunia kwa Wanawake kwa mwaka 2027, umepangwa kufanyika mwakani. 

Mwaka uliopita, DFB ilisema itapendekeza miji ya magharibi ya Ujerumani kama Dortmund, Duisburg, Dusseldorf na Cologne itumike katika mchuano huo.

Hayo ni katika juhudi zake za kuwa mwandalizi mwenza wa kombe hilo, ambalo Ujerumani pia ilikuwa mwenyeji wake mwaka 2011.