1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Scholz ataka Ukraine ipewe hakikisho la usalama

2 Juni 2023

Kansela Scholz amesema hakikisho la usalama linahitajika kwa Ukraine, kuipa uwezo kukabili kitisho kinachoweza kutokea.

https://p.dw.com/p/4S69i
Estland | Bundeskanzler Scholz in Tallinn
Picha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema Ukraine na washirika bado wako nyuma sana katika kufikia amani inayohitajika kwa Ukraine.

Ameongeza kwa kusema hatma ya hakikisho la amani la Ukraine linahitaji kuwa tofauti na lile la wanachama wa Umoja wa Kujihami wa NATO.

Amesema kutokana na hali ilivyo sasa sio tu kuendeleza uanachama wa jumuiya hiyo, bali wote kwa kila taifa walenge katika namna gani ya kuiunga mkono Ukraine.

Kansela Scholz aliongeza kwa kusema hakikisho la usalama kwa taifa hilo unahitaji kuipa uwezo Ukraine katika kukablina na kitosho kinachoweza kuitokea.

Mapema siku ya Alhamisi, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy alishinikiza takwa lake la Ukraine kuwa sehemu ya jeshi la muungano wa NATO na kuwataka wanachama wa jumuiya hiyo  kuchukua uamuzi wazi juu ya kama inaweza kuikubali Ukraine.