1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz asema Ujerumani iko tayari kuekeza Nigeria

30 Oktoba 2023

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema nchi yake iko tayari kuekeza katika gesi na madini muhimu nchini Nigeria.

https://p.dw.com/p/4YBfs
Kansela wa Ujerumani Plaf Scholz (Kushoto) na rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu wakihutubia waandishi wa habari mjini Abuja baada ya mazungumzo ya pande mbili Oktoba 29, 2023
Kansela wa Ujerumani Plaf Scholz (Kushoto) na rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu wakihutubia waandishi wa habari mjini Abuja baada ya mazungumzo ya pande mbili Oktoba 29, 2023Picha: Kola Sulaimon/AFP/Getty Images

Nigeria ni mzalishaji mkubwa wa mafuta barani Afrika. Scholz amesema hayo, wakati alipoanza ziara yake ya mataifa mawili kusini mwa Jangwa la Sahara.

"Kama ulivyosema tayari kuna nafasi nyingi, sio tu kutoka kwa gesi na mafuta ambayo kitamaduni yanahusishwa na nchi yako ila kuna nafasi kubwa sana ya kuboresha hali ila pia kuekeza kwa ajili ya baadae na hapa tunazungumzia gesi ya hydrojeni na vitu vyote muhimu kwa ajili ya uchumi vinavyoweza kuzalisha bidhaa muhimu bila kuyaharibu mazingira," amesema Scholz.

Hii ni mara ya tatu ambapo Scholz anafanya ziara katika eneo hilo katika kipindi cha miaka miwili na inafanyika wakati ambapo mizozo kwengineko duniani inaonyesha umuhimu wa eneo lenye utajiri wa nishati, ambalo Ujerumani imekuwa haijihusishi pakubwa nalo.

Rais wa Nigeria Bola Tinubu kwa upande wake amesema amefanya mazungumzo ya kina na Scholz kuhusiana na gesi na amewataka wawekezaji wa Ujerumani kuekeza Nigeria.

Kansela huyo wa Ujerumani baade leo  ataelekea Ghana.