1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz alaani shambulizi la Hamburg

10 Machi 2023

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, amelaani vikali shambulizi la ufyatuaji risasi katika ukumbi wa mikutano unaotumiwa na Mashahidi wa Jehova kwenye mji wa Hamburg.

https://p.dw.com/p/4OUSQ
Deutschland | PK Bundeskanzler Olaf Scholz
Picha: Jörg Carstensen/dpa/picture alliance

Scholz ameliita shambulizi hilo kama ''kitendo cha ukatili.''Ameandika leo katika ukurasa wake wa Twitter kwamba yuko pamoja na wahanga na familia zao, na vikosi vya usalama ambavyo vilikabiliana na opersheni ngumu. Polisi ya Ujerumani imesema watu wanane wameuawa, akiwemo mshukiwa wa uhalifu huo.

Taarifa ya gazeti la Bild imeeleza kuwa watu waliouawa ni saba na takribani watu wengine wanane wamejeruhiwa. Aidha katika taarifa yake, Mashahidi wa Yehova wameelezea kusikitishwa na shambulizi hilo la kutisha dhidi ya wafuasi wake. Polisi inalichunguza shambulizi hilo.