SiasaUkraine
Scholz alaani mashambulizi ya Urusi dhidi ya maeneo ya raia
30 Mei 2023Matangazo
Ofisi ya Scholz imesema katiaka taafisa kuwa kansela amelaani mashambulizi hayo kupitia mazungumzo ya simu na Rais Volodymyr Zelensky.
Scholz amesisitiza mshikamano na Ukraine wakati ikikabiliana na uvamizi wa shirikisho la Urusi, bila hata hivyo kutaja mashambulizi ya droni yasio kifani yaliofanywa dhidi ya majengo ya makazi mjini Moscow.
Kwa mujibu wa mamlaka ya kijeshi nchini Ukraine mapema leo Urusi imefanya mashambulizi kwa siku ya tatu mfululizo katika mji ya Kiev na kusababuisha kifo cha mtu mmoja.