1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Saudi Arabia yatuma mjumbe kwenye ukingo wa Magharibi

26 Septemba 2023

Saudi Arabia imepeleka ujumbe wake katika eneo la Ukingo wa Magharibi linalokaliwa kwa mabavu na Israel. Hatua hiyo ni ya kwanza kuwahi kuonekana kwa kipindi cha miongo mitatu iliyopita.

https://p.dw.com/p/4WopC
Rais wa Mamalaka ya Wapalestina Mahmoud Abbas katika mazungumzo na mwanamfalme wa Saudia Mohammed bin Salman
Rais wa Mamalaka ya Wapalestina Mahmoud Abbas katika mazungumzo na mwanamfalme wa Saudia Mohammed bin SalmanPicha: Thaer Ganaim/APA Images/ZUMA Press/picture alliance

Saudi Arabia iliyoingia kwenye mazungumzo na Israel, yanayosimamiwa na Marekani kujaribukurudisha mahusiano ya kidiplomasia, leo imepeleka ujumbe wake katika eneo la Ukingo wa Magharibi linalokaliwa kwa mabavu na Israel.

Soma piaSaudia yasifu "matokeo chanya" ya mazungumzo na waasi wa Houthi wa Yemen

Ujumbe huo unaongozwa nabalozi wake nchini Jordan, ambaye pia anashughulikia Mamlaka ya Wapalestina, Nayef al Sudairi, na anatarajiwa kukutana na Rais Mahmoud Abbas pamoja na mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Palestina, Riyad al-Maliki.

Saudi Arabia inasema ziara ya balozi wake huyo inanuwia kufungua njia ya kumaliza mgogoro kati ya Israel na Palestina.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW