1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSaudi Arabia

Saudi Arabia yakubali kushirikiana na China

Daniel Gakuba
29 Machi 2023

Saudi Arabia imekubali kujiunga na Muungano wa Ushirikiano wa Shanghai kama mshirika katika mjadala.

https://p.dw.com/p/4PS3q
DW Middle East - Saudi Arabia: National makeover in full swing
Picha: ATHIT PERAWONGMETHA/AFP/Getty Images

Mbali na China, washirika wengine katika muungano huo ni Urusi, India, Pakistan na nchi nne za Asia ya kati ambazo ni Kazakhstan, Kyrgyzstan, Uzbekistan na Tajikistan. Ushirika huo ulindwa mwaka 2001 kama muungano wa kisiasa, kiuchumi na kiusalama dhidi ya taasisi za kimagharibi. Shirika rasmi la habari la Saudi Arabia, SPA limesema uamuzi wa kujiunga na Muungano wa Ushirikiano wa Beijing ulichukuliwa katika kikao cha baraza la mawaziri kilichoongozwa na Mfalme Salman wa Saudi Arabia. Nchi nyingine zenye hadhi ya mshirika katika mjadala kwenye muungano huo ni Misri, Iran na Qatar.