1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Saudi Arabia yaisadia Yemen dola milioni 250

12 Februari 2024

Saudi Arabia jana Jumapili imesema kuwa imetoa msaada wa dola milioni 250 kwa serikali inayotambulika kimataifa nchini Yemen, ambayo taifa hilo la Ghuba linaunga mkono katika vita yake dhidi ya waasi wa Huthi.

https://p.dw.com/p/4cHFk
UN I Rashad Mohammed Al-Alimi
Rais wa Yemen Rashad Mohammed Al-Alimi akihutubia Kikao cha 77 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York.Picha: Mike Segar/REUTERS

Pesa hizo zinatolewa baada ya malipo ya awali ya kiasi kama hicho yaliyotangazwa mwezi Agosti, wakati serikali ya Riyadh ilipojitolea kutoa jumla ya dola bilioni 1.2 ili kupunguza nakisi ya bajeti ya serikali na kulipa mishahara kwa watumishi wa umma. Balozi wa Saudia nchini Yemen, Mohammed al Jaber amesema awamu ya pili ruzuku ya kusaidia kushughulikia nakisi ya bajeti ya serikali ya Yemen iliingizwa katika Benki Kuu ya Yemen huko Aden, kiasi cha dola milioni 250 kusaidia mishahara na malipo matumizi mengine. Serikali ya Yemen ilihamishiwa Aden, mji wa bandari wa pwani ya kusini, baada ya waasi wa Huthi wanaoungwa mkono na Iran kuuteka mji mkuu wa Sanaa mwaka 2014. Mwaka wa 2015 Saudi Arabia ilianzisha muungano wa kimataifa wa kijeshi ulionuia kuwatimua Wahuthi.