1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sasa ni hakika NATO kujitoa Afghanistan 2014

22 Mei 2012

Baada ya mkutano wa NATO (21.05.12) ,Ujerumani inajisikia ahueni kidogo. Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Guido Westerwelle ,alikuwa na shaka kutokana na msimamo wa Ufaransa kuhusu Afghanistan.

https://p.dw.com/p/14zm9
U.S. President Barack Obama is shown on large screens as the NATO Summit gets underway in Chicago, May 20, 2012. REUTERS/Larry Downing (UNITED STATES - Tags: POLITICS MILITARY)
Kikao cha mkutano wa NATO-mjini Chicago 2012Picha: REUTERS

Wasi  wasi  uliokuwapo ni kwamba  rais  wa  sasa  wa  Ufaransa  Francois  Hollande angeyaondoa  na  mapema  majeshi  ya  nchi  yake  kutoka Afghanistan. Lakini  baada  ya  mkutano  wa  NATO wasi wasi  huo  umeondoka  na  kwamba  Ufaransa  itaendelea kutoa  ushirikiano.

Mpango wa  kujitoa  wathibitishwa

Viongozi  wa  NATO  jana  waliweka utaratibu wa  kujitoa kutoka  katika  vita  ambavyo  haviungwi  mkono  na  watu wengi  nchini  Afghanistan, wakiunga  mkono  mipango  ya kukabidhi uongozi  wa  mapambano  kwa  Waafghan wenyewe  kuanzia  katikati  ya  mwaka  2013  huku wakitilia  mkazo  kuwasaidia  wakati  nchi  hiyo  ikielekea katika  kuchukua udhibiti  wa  kila  kitu.

U.S. President Barack Obama holds a news conference after the 2012 NATO Summit in Chicago at McCormick Place in Chicago, May 21, 2012. REUTERS/Larry Downing (UNITED STATES - Tags: POLITICS)
Rais wa Marekani Barack ObamaPicha: Reuters

Katika  azimio lililotolewa katika mkutano wa Chicago , rais wa  Marekani  Barack  Obama  pamoja  na  washirika  wake wa  kijeshi  wa  NATO waliidhinisha  mpango  maalum ambao  hautabadilika  wa  kujitoa  taratibu lakini  kwa utaratibu  maalum  wa  uwajibikaji kwa  kuondoa  wanajeshi 130,000 ifikapo  mwishoni  mwa  mwaka 2014.

Waafghanistan  hawatakuwa peke yao

Rais Obama  ameuambia  mkutano  huo  kuwa  wakati Waafghanistan  wanasimama  kuchukua  jukumu  la  nchi yao hawatakuwa  peke  yao.

"Wakati  Waafghanistan wanasimama, hawatasimama peke yao. Leo tumekubaliana  juu  ya  uhusiano  wa muda  mrefu wa  NATO  na  Afghanistan  kupindukia  mwaka  2014, ikiwa ni  pamoja  na  msaada  wetu  kwa  majeshi  ya  usalama ya  Afghanistan."

Kansela  wa  Ujerumani  Angela  Merkel  amesisitiza  kuwa haoni hatari yoyote, kuhusiana  na msimamo  wa  Ufaransa kwamba  huenda  kutakuwa  na hali  ya  mataifa  mengine kujitoa  kutoka  Afghanistan iwapo Ufaransa ingejitoa. Kwa hiyo NATO imethibitisha mpango wake kwa  ajili  ya Afghanistan.

French President Francois Hollande talks with German Chancellor Angela Merkel during the NATO Partners meeting at the NATO Summit, Monday, May 21, 2012, in Chicago. (Foto:Carolyn Kaster/AP/dapd) eingest. SC
Angela Merkel na Hollande wa UfaransaPicha: ap

Ufaransa pia  itasaidia

Hata  baada  ya  mwaka  2014 NATO itaendelea  kuwapo nchini  Afghanistan, kwa  kazi  ya  elimu, ushauri  na usaidizi. Waziri  wa  ulinzi  wa  Ujerumani  Thomas de Maiziere amesema:

Berlin/ Bundesverteidigungsminister Thomas de Maiziere (CDU) posiert am Mittwoch (02.05.12) in Berlin auf dem Roten Teppich zum Festakt anlaesslich des 100. Geburtstags des Verlegers Axel Springer (1912-1985). Axel Springer waere am Mittwoch 100 Jahre alt geworden. (zu dapd-Text) Foto: Maja Hitij/dapd
Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Thomas de MaizierePicha: dapd

"Hii  ina maana ya  misingi sahihi  ya kisheria kupitia  azimio la  umoja  wa mataifa, kwa ujumbe  huu  unaoongozwa  na NATO, ujumbe  ambao hautakuwa  wa  mapambano, ambao utakuwa  na  wajibu  wa  kutoa  ushauri  na usaidizi, wakati huo  huo  ukiwa  na wajibu  pia  wa kutoa  msaada  wa elimu  ambapo  ni  uwekezaji  wa  muda  mrefu."

Hata  hivyo  muda  wa  kubakia   nchini  humo  utapaswa kuidhinishwa  tena  na  bunge  la  Ujerumani  mwakani 2013.

Mwandishi : Bergmann, Christina / ZR / Sekione  Kitojo

Mhariri : Mohammed Abdul Rahman