1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sarkozy asema hatua za Macron huenda zikazua vurugu Ufaransa

16 Juni 2024

Rais wa zamani wa ufaransa Nicolas Sarkozy ameonya kwamba hatua ya kushtukiza ya rais wa sasa wa taifa hilo Emmanuel Macron ya kulivunja bunge na kuitisha uchaguzi wa mapema inaweza kuitumbukiza nchi hiyo katika vurugu.

https://p.dw.com/p/4h6lG
Nicolas Sarkozy
Rais wa zamani wa ufaransa Nicolas Sarkozy Picha: Emmanuel Dunand/AFP/Getty Images

Sarkozy, rais wa zamani anaetokea chama cha conservative aliyeitumikia Ufaransa kuanzia mwaka 2007 hadi 2012 na kubakia kuwa muhimu katika siasa za Ufaransa, amesema vurugu ambazo huenda zikajitokeza kufuatia hatua hiyo ya Macron huenda zikawa ngumu kuzisitisha. 

Macron ataka wanasiasa kuungana dhidi ya misimamo mikali

Macron aliitisha uchaguzi wa bunge kufanyika mara mbili Juni 30 na Julai 7, baada ya chama chake kushindwa na chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha Far Right National Rally RN katika uchaguzi wa bunge la Ulaya uliomalizika hivi karibuni.