1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sarajevo. Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita mjini The Hague anasisitiza kuwapata watuhumiwa wa uhalifu wa kivita Ratco Mladic na Karatzic kukabiliana na sheria.

4 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF7O

Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita amesema kuwa hana mpango wa kuhudhuria sherehe za kuadhimisha miaka kumi ya mauaji ya halaiki ya srebrenica.

Kiasi cha Wabosnia Waislamu 8,000 watu wazima na vijana waliuwawa na wanajeshi wa Serbia mnamo Julai 1995. carla del Ponte aliwaambia waandishi wa habari katika mji mkuu wa Bosnia, Sarajevo, kuwa anaweza tu kuhudhuria maadhimisho hayo, iwapo watuhumiwa wakubwa wa uhalifu wa kivita Waserbia Radovan Karadzic na Ratco Mladic watakabidhiwa katika mahakama hiyo ya umoja wa mataifa.

Sarajevo imekuwa kituo cha mwisho cha del Ponte katika ziara yake ya mataifa ya iliyokuwa Yugoslavia ya zamani kuangalia ushirikiano wao na mahakama hiyo ya kimataifa ya uhalifu wa kivita. Amesema kuwa Bosnia, Croatia na Serbia zinapaswa kufanya zaidi kusaidia kuwafikisha watuhumiwa hao wa uhalifu wa kivita mbele ya sheria.