1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SANTIAGO Dikteta wa zamani wa Chile, Augusto Pinochet, kujibu mashtaka ya wizi wa fedha

8 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF5k

Mahakama ya kukata rufaa nchini Chile imepitisha uamuzi wa kufutilia mbali kinga ya kidiplomasia ya dikteta wa zamani wa Chile, Augusto Pinochet, ili aweze kujibu mashtaka ya wizi wa fedha yanayomkabili, baada kugunduliwa kwamba ana mamilioni ya dola katika akaunti za siri kwenye benki za Marekani.

Mashtaka hayo yanaiongeza orodha ya mashtaka mengine, yakiwemo yale yaliyowasilishwa na jamaa za watu 3,000 waliotekwa nyara na kuuwawa wakati wa maongozi ya Pinochet kati ya mwaka wa 1973 na 1990. Mawakili wa Pinochet wanatarajiwa kukata rufaa juu ya uamuzi huo.