1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SANTIAGO. Augusto Pinochet sasa aweza kufikishwa mahakamani

15 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEb5

Mahakama kuu ya nchini Chile imethibitisha kwamba kiongozi wa zamani wa nchi hiyo dikteka Augusto Pinochet ameondolewa kinga ya kisheria na kwamba sasa anaweze kufikishwa mahakamani kujibu madai juu ya kuawa kwa wapinzani wapatao 120 mnamo mwaka 1975.

Utawala wa dikteta huyo ambae sasa ana umri wa miaka 89 ulipinga madai hayoa na kueleza kwamba wapinzani hao waliua kutokana na mapigano ya makundi yaliyokuwa yanapingana.