1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SANTA CRUZ: Wakimbizi wa Ki-Afrika wamezama baharini

27 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDHd

Si chini ya wakimbizi 22 wamezama kwenye pwani ya Afrika ya Magharibi walipojaribu kukimbilia Visiwa vya Canary.Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Hispania,wakimbizi hao waliotokea Mauritania na Senegal,walikuwa katika boti mbili. Kuna khofu kuwa idadi ya watu waliopoteza maisha yao,huenda ikawa kubwa zaidi,kwa sababu boti kama hizo kwa kawaida hupakia hadi watu 100.Polisi nchini Mauritania imesema,imeweza kuwazuia kama Waafrika 180 waliotaka kukimbilia Visiwa vya Canary.