1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SANA’A : Watuhumiwa 4 wa Al Qaeda mbaroni

17 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDBc

Askari wa Usalama wa Yemen wamewakamata wanachama wanne wa tawi la Al Qaeda ambao walikuwa wakipanga njama ya kufanya mashambulizi ya kigaidi mjini Sana’a.

Waziri wa Ulinzi Rashad al- Alimi amewaambia waandishi wa habari wanajeshi wa kupiga vita ugaidi waliivamia nyumba moja waliokuwa wamejibanza watuhumiwa hao katika mji mkuu wa Sana’a na kuwakamata wanne pamoja na mkururo wa silaha na mabomu.

Amelihusisha tawi hilo na mashambulizi ya mabomu yaliotegwa kwenye magari ya hapo Ijumaa dhidi ya vituo viwili vya mafuta mashariki mwa Yemen ambapo kwayo washambuliaji wanne waliuwawa pamoja na mlinzi mmoja wa usalama.