1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sadio Mane kufanyiwa vipimo vya afya Jumanne

20 Juni 2022

Vyombo vya habari Ujerumani vinaripoti kwamba mshambuliaji anayeihama klabu ya Liverpool Sadio mane, huenda akafanyiwa vipimo vya uchunguzi wa kiafya hapo Jumanne mjini Munich kabla kujiunga na mabingwa Bayern Munich.

https://p.dw.com/p/4CxXG
Sadio Mane
Picha: Anke Waelischmiller/SVEN SIMON/picture alliance

Ripoti hizo zinaarifu kwamba Liverpool na Bayern Munich wamekubaliana ada ya yuro milioni 32 ambazo huenda zikaongezeka kwa yuro milioni 9 zenginekutokana na ufanisi ataokaokuwa nao Mane hapo Allianz Arena.

Mkurugenzi wa michezo wa Bayern Hassan Salihamidzic alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusiana na kuwasili kwa Mane alisema kwamba anakuja Ujerumani.

Wachambuzi wengi wanasema kwamba usajili huu ni mkubwa kwani wachezaji wa haiba ya juu wamezoeleka kuhamia vila vya England na Uhispania.