1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rwanda imepeleka Wanajeshi Darfur

17 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEth

Kigali:

Serikali ya Rwanda leo imepeleka Wanajeshi wake wa kwanza 95 kati ya 1,756 katika mkoa wa Sudan wenye matatizo, Darfur ikiwa kama ni sehemu ya ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika (AU). Msemaji wa jeshi, Luteni Charles Karamba, amesema kuwa Rwanda itapeleka vikosi vitatu Darfur ambako vita vya wenyewe kwa wenyewe vimesababisha kuuawa kwa watu kati ya 180,000 na 300,000 na wengine millioni 2.4 hawana makazi. Luteni Karamba amesema kuwa hadi kufikia Agosti tisa operesheni hiyo itakuwa imekamilika. Rwanda hivi sasa ina Wanajeshi 392 katika mkoa wa Darfur ambao wanatekeleza harakati za ulinzi chini ya ujumbe wa amani wa Umoja wa Afrika. Wanajeshi wa Rwanda, huo ukiwa ni ujumbe wao wa kwanza wa amani, watasaidiwa na Wanajeshi 150 wa Kimarekani.