1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rwanda, Congo zinajaribu kuzuia usafiri wa mipaka yake

Sylvia Mwehozi
7 Agosti 2019

Rwanda na Congo zinajaribu kuzuwia usafiri kuvuka mipaka yao wakati maafisa wakipambana kudhibiti kusambaa kwa virusi vya ugonjwa wa Ebola.

https://p.dw.com/p/3NUvd
BG Ebola-Ausbruch im Kongo
Picha: picture-alliance/AP Photo/Stringer

Rwanda na Congo zinajaribu kuzuwia usafiri kuvuka mipaka yao wakati maafisa wakipambana kudhibiti kusambaa kwa virusi vya ugonjwa wa Ebola. Vikwazo vya kusafiri ni sehemu ya hatua zinazochukuliwa na maafisa wa Rwanda na Congo waliokutana nchini Rwanda siku ya Jumanne. Kulingana na taarifa iliyotolewa mwishoni mwa mkutano huo, watu wanaosafiri nje ya mipaka hiyo kwa sababu zisizo muhimu kama vile kuhudhuria warsha na mikutano ya kidini watahitaji vibali kutoka serikali zote mbili. Mripuko wa Ebola mashariki mwa Congo umesababisha vifo vya zaidi ya watu 1,800, Rwanda ilifunga kwa muda mpaka wake na Congo wiki iliyopita baada ya mtu mmoja kukutwa na Ebola mjini Goma, ulioko umbali wa kilomita 7 kutoka Gisenyi, ambao ni mji mkubwa wa mpakani upande wa Rwanda.