1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya kuomboleza vifo vya wanafunzi 17 kwa siku tatu

Sylvia Mwehozi
7 Septemba 2024

Rais wa Kenya William Ruto ametangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kuanzia Jumatatu baada ya watoto 17 wa shule ya msingi kufa kwa kuungua moto wakiwa bwenini.

https://p.dw.com/p/4kNk7
Shule ya msingi ya Hillside Endarasha
Shule ya msingi ya Hillside EndarashaPicha: AP Photo/picture alliance

Rais wa Kenya William Ruto ametangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kuanzia Jumatatu baada ya watoto 17 wa shule ya msingi kufa kwa kuungua moto wakiwa bwenini, kwenye shule ya msingi ya Hillside Endarasha iliyoko kaunti ya Nyeri.

Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio makamu wa Rais Rigathi Gachagua, alisema wanafunzi 70 hawajulikani walipona 27 wako hospitali. Gachagua ameuitaja mkasa huo kuwa wa kutisha na kusema kwamba kazi ya uchunguzi kwa kutumia vinasaba DNA itahitajika ili kusaidia kuwabaini wahanga na kutoa wito kwa jamii kusaidia katika kuwatafuta waliopotea.Kenya: Wanafunzi 70 hawajulikani walipo kufuatia mkasa wa moto

Taharuki imetanda miongoni mwa familia za watoto zilizokusanyika shuleni hapo zikisubiri kupata taarifa. Kulingana na jeshi la polisi, miili ya watoto iliyopatikana katika eneo la ajali imeungua kiasi cha kutotambulika.