1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ruto alikosoa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

22 Septemba 2023

Rais wa Kenya William Ruto, amelishambulia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kulitaja kuwa ‘lisilofanya kazi vizuri na lisilo na uwakilishi.

https://p.dw.com/p/4WgZs
William Ruto
Rais wa Kenya William RutoPicha: Khalil Senosi/AP/picture alliance

Rais wa Kenya William Ruto, amelishambulia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kulitaja kuwa ‘lisilofanya kazi vizuri na lisilo na uwakilishi.

Waliyoyasema viongozi wa afrika katika mkutano wa UNGA: Viongozi hao kadhaa wa Afrika wahutubia kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa akiwemo Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin Archange Toudera

Ruto amesema hayo alipoihutubia hadhara kuu ya Umoja wa Mataifa jana Alhamisi mjini New York. Ametoa wito kwa Umoja wa Mataifa.

"Ikiwa uthibitisho wowote uliwahi kuhitajika kwamba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa halifanyi kazi vizuri, halina demokrasia, halijumuishi watu wote, haliwakilishi na kwa hivyo haliwezi kuleta maendeleo ya maana katika ulimwengu wetu kama ilivyo sasa, basi kutoadhibiwa kulikoenea kwa baadhi ya watendaji katika jukwaa la kimataifa kunatoa jibu kwa hilo," alisema rais Ruto.

Ruto pia aliangazia hali nchini Haiti na akauhimiza Umoja wa Mataifa kutoa kwa dharura utaratibu wa kupeleka vikosi vya kiusalama kama sehemu ya mpango mpana wa kukabili changamoto za Haiti.