1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiKenya

Ruto aipigia upatu Kenya kuwa eneo salama kwa uwekezaji

16 Septemba 2023

Rais William Ruto wa Kenya aliye ziarani nchini Marekani ameyatembelea makampuni makubwa ya teknolojia na kuipigia upatu nchi yake kuwa eneo rafiki kwa uwekezaji licha ya serikali yake kupandisha kodi ya biashara.

https://p.dw.com/p/4WQLS
Rais William Ruto wa Kenya
Rais William Ruto wa Kenya Picha: Monicah Mwangi/REUTERS

Akitoa hotuba mbele ya makampuni hayo yenye ofisi zake mjini San Fransisco ikiwemo ile inayomiliki mitandao ya kijamii ya META na ya kuunda simu za kisasa ya APPLE, rais Ruto amesema Kenya ni eneo salama kwa uwekezaji na yenye mfumo rafiki wa kodi.

Amewaahidi wawekezaji kuwa sera zilizopo zinatabirika na serikali yake imeondoa kodi ya ongezeko la thamani kwa uwekezaji wa sekta ya teknolojia kutoka nje.

Hata hivyo wakosoaji wake wanasema serikali ya kiongozi huyo imeongeza gharama za kufanya biashara nchi humo ikiwemo kwenye sekta ya teknolojia.

Miongoni mwa nyongeza hizo ni kupandishwa maradufu ushuru wa huduma kwa makampuni ya teknolojia katika bajeti ya serikali iliyopitishwa mapema mwaka huu.