1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSudan

RSF wadai kukamata kambi ya polisi kusini mwa Khartoum

26 Juni 2023

Kikosi cha wanamgambo wenye nguvu nchini Sudan cha Rapid Support Forces (RSF) kimesema kimechukua udhibiti wa kambi moja ya polisi yenye shehena kubwa ya silaha hapo jana Jumapili.

https://p.dw.com/p/4T5SN
Sudan | Kämpfe in Khartoum
Picha: - /AFP/Getty Images

Taarifa ya RSF imesema wapiganaji wake wameikamata kambi hiyo iliyokuwa ikutumiwa na kikosi cha polisi wa akiba kusini mwa mji mkuu wa Sudan, Khartoum na mikanda ya video imewaonesha wapiganaji wake wakishangilia ndani ya viunga vya kambi hiyo.

Wengine wameonekana wakipakua makasha yaliyojaa silaha kutoka kwenye ghala moja kambini humo. Baadaye RSF ilisema imekamata magari 160 ya kubeba mizigo, mengine 75 ya kivita na vifaru 27.

Hata hivyo shirika la habari la Reuters halikuweza kuthibitisha taarifa hizo na hadi sasa hakuna ripoti zozote zilizotolewa na jeshi la Sudan wala idara ya polisi. 

Tukio hilo linaripotiwa wakati kikosi cha RSF kinajaribu kuimarisha nafasi yake kwenye mapigano makali dhidi ya jeshi la taifa hususani kwenye viunga vya mji mkuu wa Khartoum.